Home KITAIFA WAHITIMU JKT WAAHIDI UZALENDO KWA NCHI ,BAADA YA KUHITIMU MAFUNZO

WAHITIMU JKT WAAHIDI UZALENDO KWA NCHI ,BAADA YA KUHITIMU MAFUNZO

Kibaha

WAHITIMU wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamemwahidi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kulinda rasilimali na kujenga uchumi imara wa nchi ili ipate maendeleo.

Wametoa ahadi hiyo wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya JKT Operesheni miaka 60 ya Muungano kwenye kambi ya Ruvu Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Akisoma risala ya wahitimu hao Hilda Edward amesema kuwa watayatumia mafunzo hayo kwa kuifanyia nchi yao uzalendo ambao wamefundishwa kwenye mafunzo hayo ya miezi mitatu yaliyoanza Juni mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema kuwa Taifa linawategemea vijana kufanya kazi kwa weledi na uadilifu na wanapaswa kuwa wabunifu.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Brigedia Jenerali Solotina Nshushi amesema kuwa vijana hao wanapaswa kujitunza na kuacha kutumia vilevi ambavyo vitasababisha kupata matatizo ya afya ya akili na miili.

Naye mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali George Kazaula amesema kuwa vijana hao wanapaswa kutumia nidhamu kama silaha kwa kila jambo wanalolifanya.

Awali Mkuu wa kikosi hicho cha Ruvu Kanali Peter Mnyani amesema kuwa kambi hiyo pia inachukua vijana wenye mahitaji maalumu ambao nao wamehitimu mafunzo hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here