Home KITAIFA SERIKALI IMELITAMBUA DENI LA KIWIRA COAL MINE LA SHILINGI BILIONI 1.52

SERIKALI IMELITAMBUA DENI LA KIWIRA COAL MINE LA SHILINGI BILIONI 1.52

Dodoma

NAIBU Waziri wa Madini, Dk.Steven Kiruswa amesema Serikali imelitambua deni la Shilingi Bilioni 1.52 lililotokana na mapunjo ya mafao kutoka kwa waliokuwa wafanyakazi na madeni ya Wazabuni wa Mgodi wa Kiwira Coal Mine kabla ya ubinafsishaji.

Dk. Kiruswa ameyasema hayo leo Septemba 2, 2024, Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kyela Ally Mlanghila Jumbe aliyetaka kujua mahali ulipofikia mchakato wa Serikali wa kuwalipa wafanyakazi hao na kuongeza kwamba, tayari deni hilo limepelekwa Hazina baada ya uhakiki kukamilika liweze kulipwa pindi fedha zitakapopatikana.

‘’Spika, uhakiki wa madeni hayo ulibaini madai ya wafanyakazi yalikuwa shilingi bilioni 1.024 kwa wafanyakazi 893 na madeni ya wazabuni ikiwemo watoa huduma ya ulinzi yalikuwa ni shilingi milioni 496 na kufanya deni lote kuwa jumla ya shilingi bilioni 1.52,’’ amesema Dk. Kiruswa.

Amefafanua kuwa, baada ya Chama cha Wafanyakazi Mgodini (TAMICO) kuwasilisha malalamiko ya mapunjo hayo Serikalini, Serikali ilifanya ukaguzi maalum kupitia kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Novemba 2008 na baadaye Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (Internal Audit General) alihakiki madeni hayo Agosti, 2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here