Home MICHEZO WATUMISHI HOSPITALI YA MWALIMU NYERERE MABINGWA BONANZA LA KUJENGA AFYA

WATUMISHI HOSPITALI YA MWALIMU NYERERE MABINGWA BONANZA LA KUJENGA AFYA

Na Shomari Binda-Musoma

WATUMISHI wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wameibuka washindi wa jumla wa bonanza la kujenga afya.

Bonanza hilo limefanyika leo agosti 31 kwenye uwanja wa kumbukumbu ya karume kwa kufanyika michezo ya mpira wa miguu,netball,riadha,kuvuta kamba kufukuza kuku na kukimbia kwenye magunia.

Katika michezo hiyo timu ya watumishi wa hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wamepoteza mchezo mmoja upande wa riadha kwa wanaume.

Kwenye mchezo wa soka timu ya hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wameifunga timu ya RAS Mara mabao 3-2 kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1

Kwenye mchezo wa netball watumishi hao wameifunga timu ya kombaini ya Musoma goli 23-7 na kushinda pia kwenye kuvuta kamba na kukimbia kwenye magunia.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi afisa utumishi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Heven Kombe amemshukuru mganga mfawidhi wa hospital hiyo Dk.Osmund Dyagura na uongozi kwa kuandaa bonanza hilo.

Amesema ushiriki wa michezo kwa watumishi unajenga afya na inaongeza ari ya kufanya kazi na kuwaweka watumishi pamoja.

Kombe amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanaondoshwa kwa mazoezi na kuhimiza watumishi kufanya mazoezi.

Katibu wa hospitali hiyo, Recho Kajobi amesema bonanza lililofanyika litakuwa endelevu kwa kuandaa na kuwaweka watumishi pamoja.

Kwa upande wao washiriki wa bonanza hilo wamewashukuru waandaaji na kuomba kufanyika mara kwa mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here