Home KITAIFA MAADHIMISHO YA BIMA YAFANA ZANZIBAR: “SERIKALI HAIWEZI KUFUMBIA MACHO MAGARI KUKOSA BIMA”...

MAADHIMISHO YA BIMA YAFANA ZANZIBAR: “SERIKALI HAIWEZI KUFUMBIA MACHO MAGARI KUKOSA BIMA” – ZENA SAID

Zanzibar

MAMLAKA yaUsimamizi wa Bima( TIRA) kupitia ofisi ya Zanzibar leo jumamosi Agosti 31, imefanya maadhimisho ya Bima yaliyojumuisha matembezi ya hiari katika kukuza uelewa wa elimu ya bima visiwani humo.

Matembezi hayo yameanzia katika uwanja wa Mnara wa Kisonge, Michenzani mpaka uwanja wa Mao Zedong ambapo maadhimisho hayo yamefanyika.

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo ni Mhandisi Zena Said, Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar.

.Zena Said amesema “Serikali haiwezi kufumbia macho magari kukosa bima, tutafanya kazi na taasisi zingine wasiingie ili wasiweze kuingia barabarani, pia nawaasa viongozi wa serikali kukatia bima mali zao”

Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Kamishna wa Bima Tanzania Dk. Baghayo Saqware na Naibu Kamishna wa Bima Tanzania Khadija Said,Katibu Wakuu na Manaibu Katibu wa Kuu wa Serikali pamoja na wadau mbali mbali wa bima.

Matembezi ya Bima Zanzibar ni tukio la kila mwaka linaloandaliwa ili kuongeza uelewa kuhusu umuhimu Zanzibar. Tukio hili limekuwa likifanyika kwa ushirikiano wa wadau wa sekta ya Bima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here