Home KITAIFA KATA YA BWIGIRI KUPEWA MBINU YA KULINDA WANAWAKE WENYE ULEMAVU NA WATOTO...

KATA YA BWIGIRI KUPEWA MBINU YA KULINDA WANAWAKE WENYE ULEMAVU NA WATOTO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI

Dodoma

TAASISI ya Foundation for Disabilities Hope FDH imezindua mradi wa kuzuia ukatili dhidi ya Wanawake na watoto wenye ulemavu katika kata ya Bwigiri mkoani Dodoma kwa miezi sita ili kuwapa mbinu za kujilinda wasifanyiwe ukatili wa kijinsia kwenye jamii zao lengo likiwa ni kutokomeza Mila potofu dhidi ya Wanawake, Watoto na wenye ulemavu.

Hayo yamesemwa leo Agosti 31, 2024 jijini Dodoma Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Michael Salali wakati wa uzinduzi wa Mradi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na wenye ulemavu wilaya Chamwino mradi unaofadhiliwa na Shirika la Women fund Tanzania Trust.

Amesema Wanawake wanapitia changamoto lakini Wanawake wenye ulemavu wanapitia changamoto zaidi ikiwemo kubakwa, kupigwa.

“Kwahiyo tumeona tuwajengee uwezo ili wajue chakufanya wanapokutana na vitendo vya ukatili kwenye Jamii zinazowazunguka kwa kuwawezesha kujua haki za binadamu na haki zao za msingi sambamba na jamii nayo ijue chakufanya kuishi na Watu wenye ulemavu,” amesema Salali

“Watu wenye ulemavu wanatakiwa washirikishwe mipango yote ya maendeleo kwenye Jamii zao hivyo tunatoa elimu ya haki za binadamu ili watambue haki zao za msingi.

“Hasa tunaongea na jamii tunawapa uelewa Wanawake na watoto wakiwa ndio walengwa wetu wakuu ili kwamba wapaze sauti zao kunapotokea vitendo vya ukatili kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama ili hatua stahiki zichukuliwe na wapate ufumbuzi pia,” amesema.

Aidha Mkurugenzi huyo ameomba ushirikiano wa Wananchi wa Kata ya Bwigiri ili FDH wafanikishe malengo ya mradi huo

Katibu wa Msikiti wa Kata ya Bwigiri Ustadhi Omary Mtambi ameshukuru kwa mradi huo kufanywa katika Kata hiyo nakusema kazi itakayotekelezwa na mradi huo itawasaidia kazi viongozi wa dini ambapo jukumu lao ni kuangalia ustawi wa maisha ya makundi yote ikiwemo watu wenye ulemavu.

“Watu wenye mahitaji maalumu hususani walemavu hukimbilia kuomba msaada katika nyumba za ibada hivyo nawapongeza wote waliofikiria kuleta Mradi huu katika maeneo yetu ya Bwigiri.

“Tunaahidi kutoa ushirikiano mkubwa hususani kipindi hiki ambacho kumekuwa na vitendo vinginvya watu kufanyiwa ukatili,”

Ustadhi Mtambi amesema Taasisi ya FDH kwa kushirikiana na serikali imeonyesha kuwa mstali wa mbele kupinga vitendo vya ukatili kwenye Jamii.

Aidha Ustadhi Mtambi ameipongeza serikali kwa kuendelea kupinga vitendo vya ukatili kwa kundi la watu wenye ulemavu nchini.

Aidha Mratibu wa Mradi wa kuzuia ukatili dhidi ya Wanawake na watoto wenye ulemavu Glory Mbowe.amesema mradi huo pia utahusisha na viongozi wa dini ambao pia huusika katika kuwahudumia watu wenye ulemavu ili nao washiriki kuzuia ukatili dhidi ya Wanawake na watoto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here