Home KITAIFA SERIKALI KUENDELEZA MJADALA NA KAMPUNI ZA NISHATI ZA KIMATAIFA.

SERIKALI KUENDELEZA MJADALA NA KAMPUNI ZA NISHATI ZA KIMATAIFA.

Dodoma.

SERIKALI inaendelea na majadiliano na Kampuni za Nishati za Kimataifa kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa kuchakata na kusindika Gesi Asilia ili kuwa kimiminika-LNG na yakikamilika Serikali itaupeleka kwenye hatua inayofuata.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alipokuwa akijibu swali bungeni kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko leo Alhamisi, Agosti 29, 2024.

Swali hilo la msingi limeulizwa na Aida Joseph Khenani (Mbunge wa Nkasi Kaskazini) ambaye alitaka kujua ni lini Mkataba kati ya Tanzania na Wawekezaji wa Gesi Asilia wenye thamani zaidi ya sh. 70 Trilioni utaletwa Bungeni kuridhiwa.

“Mradi wa LNG ni mradi wenye manufaa makubwa kwa Taifa na majadiliano haya ni muhimu, ndio yatakayoweka msingi wa kodi, mirabaha pamoja na ulinzi wa Tanzania kunufaika kiuchumi. Hivyo suala la mradi wa LNG ni kipaumbele kwa Serikali,” amesema Kapinga.

Kuhusu suala la kuagiza gesi ya LPG kwa mfumo wa uagizaji kwa pamoja, jambo hili linaendelea kuchakatwa, pia Serikali inaendelea na hatua za ujenzi wa gati katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuwezesha Meli kubwa kushusha gesi ya LPG.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here