Home AFYA MUHIMBILI YAANZA KAMBI MAALUM YA UPASUAJI REKEBISHI

MUHIMBILI YAANZA KAMBI MAALUM YA UPASUAJI REKEBISHI

Dar es Salaam

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH)imeanza kambi maalum ya upasuaji rekebishi (Reconstructive Surgery) kwa kushirikiana na wataalam bingwa kutoka San Francisco Marekani.

Kambi hiyo inafanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 26 hadi 30 Agosti 2024 na inatoa matibabu ya upasuaji kwa wagonjwa wenye changamoto mbalimbali za kiafya, hususani kwenye maeneo ya uso, kichwa, mdomo, shingo, pamoja na majeraha ya mikono.

Akizungumza wakati wa kufungua kambi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Mohamed Janabi amesema ujio wa wataalam hao kutoka nje ni sehemu ya mpango mkakati wa hospitali na Wizara ya Afya katika kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.

“Kambi hii ni fursa muhimu kwa wagonjwa kupata matibabu ya kibingwa sambamba na wataalam wetu kuongeza ujuzi na kubadilishana uzoefu wa mbinu mpya za upasuaji wa kisasa,” amesema Profesa Janabi.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Upasuaji Rekebishi (MNH), Dk. Ibrahim Mkoma, amefafanua kuwa zoezi la uchunguzi wa awali kwa wagonjwa tayari limeanza na watakao bainika kuwa na hitaji la upasuaji maalum wataingizwa kwenye orodha ya matibabu kwa ajili ya upasuaji.

Wataalam hao wameambatana na wafadhili kutoka ReSurge International kutoka nchini Marekani, Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na kutoa msaada wa upasuaji rekebishi katika nchi zinazoendelea ambapo ujio wao Muhimbili ni sehemu ya jitihada hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here