Home KITAIFA RAIS MWINYI:TAKUKURU NA ZAECA ONGEZENI USHIRIKIANO.

RAIS MWINYI:TAKUKURU NA ZAECA ONGEZENI USHIRIKIANO.

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezisihi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kuongeza ushirikiano katika ufanisi wa kazi zao.

Dk. Mwinyi ametoa nasaha hizo leo Agosti, 27 jijni Dar es Salaam Ikulu, Zanzibar, alipozungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, aliyefika kujitambulisha kufuatia uteuzi wake uliofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni.

Rais Dk. Mwinyi amezishauri taasisi hizo mbili kuzidisha ushirikiano hasa kwenye miradi ya kimkakati ya maendeleo kwa maslahi ya taifa.

Akizungumza kwa wakati huo, Chalamila amemuahidi Rais Dk. Mwinyi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya ZAECA na TAKUKURU katika kufanikisha majukumu ya taasisi hizo.

Vilevile, amesifu na kupongeza juhudi za maendeleo makubwa zilizofikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Mwinyi.

Amesema, mbali na majukumu mengine waliyonayo, TAKUKURU na ZAECA imekuwa rahisi kwao kushirikiana, hasa katika kudhibiti wahalifu wa pande mbili za Muungano wanaojaribu kukimbilia mipaka ya Bara na Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here