Home KITAIFA RAIS DK. SAMIA AREJEA NCHINI, AWASILI NA KUPOKELEWA UWANJA WA NDEGE KIA...

RAIS DK. SAMIA AREJEA NCHINI, AWASILI NA KUPOKELEWA UWANJA WA NDEGE KIA – KILIMANJARO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mkoani Kilimanjaro tayari kwa kuelekea mkoani Arusha ambapo ni Mgeni Rasmi kwenye Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kitakachofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) Agosti, 28 2024.

Dk. Samia amewasili uwanjani hapo akitokea nchini Kenya ambapo alihudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Agosti, 27 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here