Home KITAIFA SHUGHULI ZA BINADAMU CHANZO CHA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

SHUGHULI ZA BINADAMU CHANZO CHA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Magreth Katengu, Dar es salaam

IMEELEZWA kuwa uharibifu wa Ardhi, uharibifu wa vyanzo ya Maji, ukataji Miti ovyo na uharibifu wa misitu,upotevu wa makazi ya wanyamapori na bayoanuai; athari za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mifumo-ikolojia ya Pwani na baharini; uharibifu wa ardhi oevu; uchafuzi wa mazingira; na kuenea kwa viumbe vamizi zinachangia kuathiri Sekta ya Uchumi.

Hayo yamesemwa leo Agosti 26,2024 Jijini Dar Es Salaam na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk.Ashatu Kijaji Katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari amesema Changamoto hizo zimekuwa zikiathiri Sekta ya Uchumi ikiwemo Kilimo, Uvuvi, Utalii, Ustawi wa Jamii na Viumbe Hai hivyo ni muhimu kuongeza jitihada za kukabiliana na Changamoto hizo.

“Mazingira na Maliasili ni Msingi wa Uhai wetu, Hivyo usimamizi wa hifadhi za rasilimali hizi ni suala la kupewa kipaumbele lenye umuhimu wa kipekee, hivyo Nchi yetu imekuwa ikihakikisha ukiweka mikakati ya kukabiliana na matumizi ya Nishati Chafu ikiwemo Kuni na Mkaa ambayo husababishwa na Ukataji wa Miti hovyo,” amesema Dk.Kijaji.

Amesema Serikali inatarajia kuratibu Mkutano wa Viongozi na Wataalam na Wadau wa Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko tabianchi , Utakaofanyika Septemba 10 ,2024 Jijini Dodoma Katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa na Wadau zaidi ya 1000 kutoka Wizarani, Taasisi za Kiserikali, Mashirika na Umma, Sekta Binafsi, vyuo vya Elimu ya Juu na Asasi zisizo za Kiserikali.

Dk. Kijaji amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,kwa jitihada anazofanya kuimarisha hifadhi na usimamizi wa Mazingira Nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here