Home AFYA MGONJWA WA 13 KUPONA SIKOSELI BMH AMSHUKURU MAMA SAMIA

MGONJWA WA 13 KUPONA SIKOSELI BMH AMSHUKURU MAMA SAMIA

Na Mwandishi wetu

MGONJWA wa 13 kupona ugonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Jonester Peleka, mwenye umri wa 10, amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa huduma ya matibabu.

Akizungumza leo Agosti, 26 2024 wakati wa dhifa ya kuruhusiwa BMH , Jonester, amesema anamshukuru Rais kwa kugharamia matibabu yake.

“Namshukuru pia Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Prof Makubi na timu yake yote kwa huduma hii. Nimehudumiwa vizuri toka nilipofika hapa,” amesema Jonester.

Kwa mujibu wa mama yake mzazi, Bahati Mbogo, amepokea taarifa kutoka kwa majirani zake kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma inatoa matibabu ya sikoseli.

“Majirani zangu waliona kwenye TV kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa wanatibu sikoseli ndiyo nikamleta mwanangu,” amesema BBahati, ambaye ni mkazi wa Bigwa Kisiwani, Morogoro.

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Damu BMH, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu, Stella Malangahe, amesema Jonester alipandikizwa uboho, ambayo ni matibabu ya sikoseli, tarehe 16 Julai, mwaka huu.

“Tumemruhusu mgonjwa wetu wa 13 kupona ugonjwa wa sikoseli siku ya leo. Tunawashukuru wazazi wake kwa kutuamini,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here