Home KITAIFA WANANCHI MUSOMA VIJIJINI WATAKIWA KUONGEZA KASI UJENZI WA SEKONDARI MPYA NA MAABARA

WANANCHI MUSOMA VIJIJINI WATAKIWA KUONGEZA KASI UJENZI WA SEKONDARI MPYA NA MAABARA

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa Kata 21 kwenye jimbo la Musoma vijijini wameombwa kuendelea kuchangia ujenzi wa sekondari mpya na maabara kwenye maeneo yao.

Maombi ya kuongeza kasi ya kuchangia yametolewa jana agosti 23 na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo kutokana na mabadiliko ya mfumo wa elimu.

Amesema kasi ya ujenzi wa sekondari mpya unapaswa kuendana na ujenzi wa maabara tatu (3) za masomo ya sayansi (physics, chemistry & biology laboratories) kwenye kila sekondari ya Kata

Muhongo amesema mabadiliko mapya ya mfumo wa elimu nchini yatahitaji ongezeko kubwa la shule za sekondari.

Amesema mabadiliko hayo ni kwamba wanafunzi wa shule za msingi watasoma hadi darasa la sita (Std VI), na wote wataendelee kupata elimu ya sekondari hadi Kidato cha Nne (Form IV).

Mbunge Muhongo amesema kwa sasa idadi ya sekondari za Kata/serikali ni 26,sekondari za madhehebu ya dini 2 huku idadi ya sekondari zenye kidato cha V & VI
(High Schools) ni Kasoma High School
Inafundisha masomo ya “arts” pekee

Amesema High Schools mbili zimepata usajili wa kufundisha masomo ya sayansi ambazo ni Suguti na Mugango High Schools ambapo maabara tatu za masomo ya sayansi zipo na mabweni yapo

Ameongeza kuwa ukamilishaji wa sekondari zilizoanzwa kujengwa miaka kadhaa iliyopita na wananchi wakishirikiana na viongozi wao unaendelea.

“Sekondari mpya hizo zinajengwa vijijini Kisiwa cha Rukuba,Muhoji serikali imeanza kuchangia pamoja na Nyasaungu.

“Sekondari mpya zinazoanza kujengwa mwaka huu kwa kutumia michango ya fedha na nguvukazi za wananchi na viongozi wao ni Chitare, Kataryo, Kiriba, Mmahare, na Nyambono,”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here