Chalinze
WANAFUNZI wa shule tano za msingi na moja ya Sekondari ya Kata ndani ya Kata ya Msoga wameanza kambi maalumu ya kujiandaa na mitihani yao inayotaraji kufanyika hivi karibuni.
Hayo yamebainishwa Agosti 22 2024,na Diwani wa Kata hiyo Hassani Mwinyikondo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi ya kata wakati akikabidhi mchango wa vyakula Afisa Elimu Msingi Miriamu Kihiyo, hatua inayolenga kuwawezesha kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Mwinyikondo amesema hatua hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anayoielekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu ambayo katika awamu ya sita imekuwa ikiendelea kufanya vizuri zaidi.
“Nimeunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu, kuhakikisha wanafunzi wanaokaa kambi itayowawezesha kufanya vizuri kwenye mitihani yao,” amesema Mwinyikondo.
“Namshukuru Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete (Waziri wa Nch Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na wenye Ulemavu) ambae amekuwa msaada mkubwa katika kusukuma hatua za maendeleo jimbo katika sekta mbalimbali,” amesema Mwenyekiti huyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Kihiyo alimpongeza Mwinyikondo kwa msaada alioutoa wa mchele, unga, mihogo na nyanya utaosaidia kwa kiwango kikubwa katika kifanikisha Wanafunzi kupata lishe Bora ili wafanye vizuri katika masomo yao.
“Pia namshukuru Mbunge wetu Ridhiwani Kikwete kwa kazi kubwa anayoendelea kuwatumikia wanaChalinze, tunashuhudia mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali,” amesema Kihiyo.
Abdul Tengwe Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Changa wameshukuru kwa msaada huo, huku
Omary Kisina Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Msoga akieleza kwamba msaada huo sio wa kisiasa, bali unalenga kuendelea elimu.