Home KITAIFA MAADHIMISHO YA WIKI YA AZAKI KUFANYIKA ARUSHA SEPTEMBA 9 HADI 13,2024

MAADHIMISHO YA WIKI YA AZAKI KUFANYIKA ARUSHA SEPTEMBA 9 HADI 13,2024

Esther Mnyika,Dar es salaam

TAAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Foundation for Civil society(FCS), inatarajia kufanya Maadhimisho ya wiki ya Azaki Arusha kuanzia Septemba 9hadi 13 ,2024 Jijini Arusha ambapo washiriki zaidi 500 wanatarajiwa kuhudhuria .

Akizungumza leo Agosti 23, 2024 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa FCS)Justice Rutenge amesema Wiki hiyo itaongozwa na kauli mbiu isemayo “sauti Dira na thamani”kwani maneno hayo yana mlengo mkubwa na tukio la nchi ya Tanzania kuhusu Uchanguzi unaotarajiwa kuanza Novemba mwaka huu huvyo watajadiliana kiundani juu ya tukio hilo.

” Maadhimisho ya Wiki hiyo ya Azaki yatakuwa ya tofauti na kipekee sanaa kwani tutatoka kwenda kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo walemavu, bodaboda, kufanya mahojiano nao kujua changamoto zao na nini wanachohitaji kutoka katika serikali yao wanapoelekea kwenye uchaguzi wafanye maamuzi sahihi;” amesema.

Amesema siku hizo watakazokutana na wadau mbalimbali kwa kuwa Mwakani wanatarajia kuzindua dira ya Taifa 2050 ambayo ni fursa inakuja mara moja baada ya miongo mitatu katika kuandaa dira ya Taifa hivyo ni muhimu sauti za wananchi kusikika ili tuondoke kwenye tamaduni ya namna hii mipango ya Serikali kuandaliwa na jopo la wataalamu wachache ambao wanachukua mawazo yao wao wenyewe pasipo kupata maoni ya wananchi wenyewe.

“Dira yetu lazima tulinganishe na nchi nyingine kabla haijatengenezwa inapaswa itokane na sauti,mawazo,mtazamo na maoni ya wananchi ndiyo maana tunasema sauti ni kipengele muhimu kwenye kauli mbiu ya wiki ya Azaki,”amesema.Rutenge

Rutenge amebainisha kuwa dira yenyewe ifike sehemu kama nchi wanakubaliana kuhusu maoni ya watanzania namna wanavyotaka iwe licha ya tofauti zetu za kidini ,kiumri na kijinsia kichama mwisho wa siku ni lengo linakuwa moja tu ni muhimu sana tutaiangazia dira kwenye tukio letu la mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu thamani ni jambo linasahaulika sana inaamanisha kwamba tunawezaje kutoa thamani ya maono tuliyojiwekea kama Taifa hivyo wiki ya Azaki ni thamani itapewa ushirikiano katika sekta,nyanja na watu wa aina mbalimbali ili kila mtu ashiriki katika mchakato wa Dira ya maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya wiki ya Azaki,Nesia Mahenge amesema wiki ya asasi za kiraia(Azaki) imekuwa na utamaduni wa. kawaida kukutana kila mwaka kwa lengo la kubadilisha mawazo na kuangazia changamoto za taifa kisha kuzipatia ufumbuzi na kupeleka maoni yao yakashughulikiwe na serikali.

‘Tunaposema mashirikiano katika sekta zote ni kuangalia sekta ya Azaki asasi za kiraia na kwa upande wa Serikali,sekta binafsi na wadau wa maendeleo kwa ujumla namna gani tutashirikiana kuleta maendeleo nchini Tanzania,” amesema Nesia

Wiki ya Azaki ni mwaka wa sita tunaadhimisha tunajivunia kila.mwaka kuendelezaa huu utamaduni watu zaidi ya 500 watahudhuria katika maadhimisho yao wakiwemo serikalini,watu binafsi na makundi mbalimbali kutoka sekta za kiraia

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Ubongo Kids,Mwasi Wilmore amesema wanayofuraja ya kuwa miongoni wa wadhamini wa Wiki hiyo kwani wanatambua shughuli kubwa wanazozifanya

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here