Home KITAIFA ALIYEPOOZA NA KUSHINDWA KUTEMBEA KWA MIAKA 7 ASAIDIWA FIMBO NA ASKARI KATA...

ALIYEPOOZA NA KUSHINDWA KUTEMBEA KWA MIAKA 7 ASAIDIWA FIMBO NA ASKARI KATA GENUINE KIMARIO

Na Shomari Binda-Serengeti

ASKARI Kata wa Kata ya Kisangura iliyopo wilayani Serengeti Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Genuine Kimario ameendelea kufanya jitihada za kuwafikia wenye uhitaji kwenye eneo analo lisimamia na kuwatafutia msaada.

Kimario amemfikia Emanuel Bhoke wa Kijiji cha Kisangura aliyeshindwa kutembea kwa miaka 7 kutokana na ugonjwa wa kupooza na kumsaidia fimbo za kutembelea

Amepokea msaada huo kutoka kwa askari huyo Emanuel amemshukuru na kudai amekuwa akipata shida ya kutembea na huo umekuwa msaada mkubwa kwake.

Amesema mazingira anayoishi kijijini sio mazuri na alikuwa hana uwezo wa kununua fimbo hizo kuweza kumsaidia kutembea na sasa amepata unafuu.

Emanuel amesema kwa sasa anao uwezo wa kutoka nyumbani na kufanya mazoezi ikiwa ni pamoja na kutembelea ndugu na jamaa kuweza kuwasalimia

” Namshukuru sana askari Kata kwa jitihada zake na kuweza kunifanikishia kupata msaada huu wa ” magongo” yaliyoweza kunisaidia kutembea.

” Kwa sasa nnauwezo wa kufanya mazoezi na kutembelea ndugu na jamaa na kuweza kuwasalimia kwa kweli namshukuru sana na Mungu amzidishie na amuongoze vyema kwenye kazi yake”amesema

Askari huyo amekuwa akijulikana kwa juhudi zake za kuunganisha jamii na kutoa msaada pale inapohitajika hasa kwa makundi yenye uhitaji maalum.

Amejenga uhusiano mzuri na wakazi wa Kisangura na kupitia nafasi yake kama afisa wa polisi amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha usalama na ustawi wa jamii unaboreshwa.

Diwani wa Kata ya Kisangura na Makamu Mwenyekiti wa Halmashari ya Serengeti Samson Ryoba amesema Kimario ameonyesha kwamba polisi si tu walinzi wa raia na mali zao bali pia ni wahudumu wa jamii wenye dhamira ya kusaidia na kuboresha maisha ya wale wanaowahudumia.

Amesema huo ni mfano mzuri wa jinsi viongozi wa umma wanavyoweza kutumia nafasi zao kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii na kwa kutambua mchango wake tayari walishampa tuzo.

Kwa upande wake askari huyo wa Kata ya Kisangura Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Genuine Kimario amesema ni utamaduni wake kuifikia jamii anayoisimamia kwa kazi yake na sio kwa ukamataji bali kusaidiana pia kwa masuala ya kijamii.

Amesema pale anapofika kwenye jamii na kukutana na changamoto uwashirikisha wadau mbalimbali na kuweza kusaidia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here