Home KITAIFA KASEKENYA AWATAKA MADEREVA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

KASEKENYA AWATAKA MADEREVA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Arusha

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Kasekenya amewataka madereva wa Serikali kufanya kazi kwa weledi ili kufikia tija na kupunguza ajali.

Akifunga kongamano la tatu la madereva wa Serikali Agosti 21 2024 jijini Arusha Naibu Waziri huyo amemtaka kila dereva kujipima kutokana na kazi anayoifanya ili kukidhi mahitaji ya Serikali, jamii na taifa kwa ujumla.

” Fahamuni mnajukumu kubwa kitaifa kuhakikisha usalama wa viongozi, wataalam na jamii hivyo zingatieni na kuheshimu sheria za barabarani na kuhakikisha mnakuwa kielelezo bora kwa jamii”, amesema.

Amezungumzia umuhimu wa madereva kuwa na nidhamu, ubunifu, tabia ya kujiendeleza kitaaluma na kutunza siri ili kuleta tija na ufanisi katika utumishi wa umma.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itaendelea kukilea chama cha madereva ili kikuwe na kufikia malengo na kuhimiza madereva wengi kujiunga na chama hicho ili kunufaika na fursa zilizopo.

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala wa Wizara ya Ujenzi Mrisho Mrisho amesema zaidi ya madereva 1600 wameshiriki kongamano hilo na kujifunza stadi za ufundi, udereva, uwekezaji na ubunifu hali itakayowawezesha kufanya kazi kwa tija na ufanisi.

Chama cha madereva wa Serikali (CMST), kilianzishwa miaka nane iliyopita na kinawanachama zaidi ya 7,200 nchini kote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here