Home MICHEZO KAMATI YA MAANDALIZI AFCON 2027 YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

KAMATI YA MAANDALIZI AFCON 2027 YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

Dar es Salaam

KAMATI ya Taifa ya maandalizi ya fainali za ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2027 imekutana leo Agosti 22, 2024 Jijini Dar Es Salaam kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kupitia na kuridhia mapendekezo ya uundwaji wa kamati ndogo pamoja na Sekretarieti ya Kamati hiyo.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mhandisi Leodgar Tenga imepitisha kamati hizo ambazo ni kamati ya usimamizi wa miundombinu, mawasiliano, fedha, tiba na “Doping” ,uendeshaji wa matukio, ulinzi na usalama, (sheria, matangazo, masoko na biashara), teknolojia ya mawasiliano ya habari ,kamati ya uidhinishaji na watoa huduma.

Ikumbukwe kwamba Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here