Home KITAIFA KITABU CHA KURUDI KWA YESU NA MFUMO WA KIDIGITALI UUZAJI VITABU KUZINDULIWA

KITABU CHA KURUDI KWA YESU NA MFUMO WA KIDIGITALI UUZAJI VITABU KUZINDULIWA

Dar es salaam

ASKOFU wa Kanisa la The Truth Ministries Nation Aurelian Ngonyani amesema kutokana na watu kuwa na shughuli nyingi na kutokuwa wasomaji wa vitabu ni vyema mbinu mbadala ya kidigital itumike ili kusaidia kila mmoja apate maarifa kwa gharama nafuu.

Akizungumza leo Agosti 21,2024 Jijini Dar es salaam katika hafla ya Uzinduzi wa kitabu cha kurudi kwa Yesu na Mfumo wa kidigitali wa uuzaji wa vitabu kwa gharama nafuu .

“Kama sehemu ya mchakato wa uandishi nilifanya utafiti kidogo kuhusu usomaji wa vitabu Tanzania na kubaini kuwa wasomaji ni wachache sana kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu rahisi inawezesha kila mtu kuwa msomaji na ajiongezeee maarifa ili kusaidia wote wanufaike nilitafuta njia hii na kuanza kuweka kitabu changu hiki kwa sauti hata wale wasioona wapate ujumbe,” amesema Askofu

Askofu amebainisha kuwa kitabu hicho ambacho kimepewa jina la “Kurudi kwa Yesu” kitauzwa kwa shilingi elfu 5000 pekee kwa njia ya Mtandao katika mifumo ya sauti( audio) na nakala Tete( pdf) na wale watakaohitaji kilichochapwa ni Tsh 25000.

Askofu Ngonyani amesema kuwa kitabu hicho kimekusanya alama za nyakati kuelekea utimilifu wa unabii wa siku ambapo matukio hayo kwa sasa yameendelea kukithiri ikiwemo Mmonyoko wa maadili kuwepo kwa mafundisho ya uongo watu kujipitia fedha ambapo katika Biblia imeandika kipawa alichopewa mtu kubariki wengine atoe bure.

Amesema kwamba kitabu hicho amekiandika baada ya kufanya utafiti kwa muda wa miaka 20 katika Nchi ambazo matukio yaliyoandikwa katika bibliayaliyoekea ambapo baadhi ya Nchi hizo ni pamoja na Misri,Jordan,Uturuki,Israel,Ugiriki,Ufaransa,Ureno,na Italia kupitia Kampuni yake ya AUMARK.

Aidha amesisitiza kuwa kwa kutumia Wahandisi wa kitanzania ,amefanikiwa kuunda Mfumo rahisi wa uuzaji wa Vitabu unaotumia msaada wa akili Mnemba “Artificial Intelligence “(AI) ambapo mtumiaji wa simu janja( Smart Phone) anachopaswa kufanya ni kuhifadhi namba ya simu nakutumia neno “Hellow au habari” kisha Mfumo utamkaribusha katika duka la Vitabu la kidigitali na utampeleka katika duka la “Ngonyani Store”

Aidha ameongeza kuwa kitabu hicho Cha Kurudi kwa Yesu kina kurasa 225,kimechakatwa na kuwekwa katika Mfumo wa sauti(audio) na nakala Tete( PDF ili kila mtu aweze kukipata kiganjani mwake kupitia Mfumo uliozinduliwa

Maudhui ya kitabu hiki ni muhimu kwa Kila mtu kuyapata kwa kuwa yanafunua kweli za msingi kuhusu Maisha ya wanadamu ya sasa na baadae,kinajibu maswali wanayoumiza vichwa vya watu wengi kama vile,tukio la Kurudi Yesu,kipindi Cha Mpinga kristo,Hatma ya Msikiti wa Al-aqsa na kujengwa kwa Hekalu la Tatu la Yerusalem,pamoja na kuweka Wazi matukio makuu ya Taifa la Israel.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here