Home KITAIFA JESHI LA POLISI MKOA WA MARA RAKAMATA WAHALIFU 357 KWA KIPINDI CHA...

JESHI LA POLISI MKOA WA MARA RAKAMATA WAHALIFU 357 KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA

Na Shomari Binda-Musoma

JESHI la polisi mkoani Mara linawashikilia watuhumiwa 357 waliokamatwa kwa tuhuma za makosa mbalimbali wakiwemo wanaojishughulisha na uvuvi haramu.

Akizungumza Agosti, 16 2024 na Waandishi wa Habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Mara Salim Morcase amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni iliyofanyika kipindi cha mwezi julai.

Amesema katika oparesheni hiyo watuhumiwa 28 waliokamatwa walifikishwa Mahakamani ambapo kesi 8 zilipata mafanikio kwa watuhumiwa kuadhibiwa kwa makosa mbalimbali.

Kamanda Morcase amesema katika oparesheni hiyo vilikamatwa pia vifaa vya uvuvi haramu zikiwemo nyavu aina ya makokoro pisi 30,kupatikana kwa pombe moshi ya gongo na watumiaji na wasafirishaji wa dawa za kulevya.

Kwa upande wa mifugo kamanda Morcase amesema wamefanikiwa kuokoa mifugo iliyoibwa sehemu mbalimbali zikiwemo ng’ombe 23,mbuzi 5,kondoo 2 na watuhumiwa 17 wamekamatwa.

Kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoani Mara amesema katika oparesheni hiyo wamefanikiwa kukamata pikipiki 2,tv 4 na vifaa mbalimbali vikiwemo vya majumbani.

” Oparesheni hii ya mwezi julai imekuwa na mafanikio makubwa na ni endelevu katika kupambana na uhalifu na wahalifu.

” Oparesheni hii ni endelevu na yeyote anayetaka kujaribu kuja kufanya uhalifu mkoa wa Mara ajue ataishia mikononi mwa jeshi la polisi,”amesema.

Aidha kamanda Morcase ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za wahalifu kwa kuwa wanaishi kwenye jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here