Home KIMATAIFA WAZIRI KOMBO KUSHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA SADC, HARARE

WAZIRI KOMBO KUSHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA SADC, HARARE

Zimbabwe

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasili Harare, Zimbabwe kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 13 na 14 Agosti, 2024.

Mkutano huo wa Mawaziri ni sehemu ya mikutano ya awali kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Agosti, 17 2024 nchini Zimbabwe.

Mkutano wa Mawaziri ulitanguliwa na kikao cha Makatibu Wakuu wa SADC kilichofanyika tarehe 8 hadi 11 Agosti, 2024 nchini humo ambacho kilijadili na kufanya maandalizi ya nyaraka mbalimbali zitakazo pokelewa na kujadiliwa na mkutano huo wa Mawaziri.

Baada ya kuwasili nchini Zimbabwe, Kombo amepokelewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zimbabwe, Balozi IGP (RTD) Simon Sirro na kufanya kikao na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki katika mikutano ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC.

Mawaziri wengine watakaoshiriki mkutano huo ni pamoja na; Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu, Zanzibar, Ali Suleiman Ameir.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here