Dodoma
SHIRIKA la Maendeleo la Uholanzi la SNV kwa kushirikiana na Farm Africa wamezindua rasmi mradi wa kuwawezesha wakulima wadogo kwa usalama wa chakula na kustahimili hali ya hewa (NOURISH Tanzania).
Pia mradi huo wa miaka mitano (2024-2028) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Norway (Norad) wenye lengo la kufikia usalama wa uhakika wa chakula kwa kaya 168,000 za wakulima wadogo (SHF) katika mikoa ya Sumbawanga, Songwe, Dodoma, Manyara na Singida.
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya chakula
na lishe kutoka wizara ya kilimo Aradius Kategama amesema serikali inaunga mkono mchango unaotolewa na sekta binafsi katika suala zima la kilimo na kwamba itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa maslahi ya Taifa.
Ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi huo Tanzania wenye lengo la kuongeza lishe nchini kwa kuanzia mikoa hiyo tajwa unaotekelezwa kupitia shirika la SNV.
Amesema kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali ni muhimu kuhakikisha matokeo yanapatikana ili kuondokana na umaskini
“Mtazamo wa mradi wa NOURISH wa kutumia mawasiliano ya mabadiliko ya tabia ya kijamii na kufanya kazi na takwimu za jamii za mitaa zinazoaminika kutoa elimu na uhamasishaji unaozingatia lishe, mienendo ya kaya na matumizi ya chakula inaweza kusababisha mazoea bora ya chakula na matokeo bora ya afya,’’
‘’Zaidi ya hayo, kwa kuboresha uhusiano kati ya wakulima, wasindikaji, na masoko, tunaweza kupunguza hasara baada ya kuvuna, kuimarisha ubora na upatikanaji wa chakula, na kuhakikisha kuwa chakula zaidi kinawafikia walaji,”amesema.
SNV ni mshirika wa maendeleo wa kimataifa, aliyejikita mizizi katika nchi za Afrika na Asia ambako inafanya kazi na uzoefu wa miaka 60 na timu ya takriban watu 1,600, ni dhamira ya SNV kuimarisha uwezo na kuchochea ushirikiano ambao hubadilisha mifumo ya kilimo ya chakula, nishati, na maji ili kuwezesha maisha endelevu na ya usawa zaidi kwa wote.
Pia inafanyakazi katika ofisi za Dodoma, Arusha, Dar es Salaam, Mwanza na Sumbawanga, na kushirikiana na watu katika mikoa 23 kote nchini,