Home AFYA HOSPITALI YA TEMEKE YAZINDUA KITUO CHA KUSAFISHIA DAMU NA MAGARI MAWILI PAMOJA...

HOSPITALI YA TEMEKE YAZINDUA KITUO CHA KUSAFISHIA DAMU NA MAGARI MAWILI PAMOJA NA VIFAA VYA WAGONJWA

Dar es salaam

WANANCHI wameendelea kuhimizwa kufanya Mazoezi kwa bidii na kupunguza hali ya ulaji wa vyakula usiofaa ili kusaidia kuepukana na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo Sukari,Shinikizo la Damu, moyo mkubwa na Afya ya akili ambayo yamekua yakiongezeka kila siku na kuwa tushio kwa kusababisha vifo vya watu.

Ushauri huo umetolewa leo Agosti 12,2024 na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda akimwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwenye Uzinduzi wa Kituo Cha Kusafishia Damu wagonjwa wa Figo, pamoja na kupokea vifaa mbalimbali ikiwemo gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) pamoja na gari la kukubea watumishi ikiwa lengo ni kuboresha utoaji wa huduma hospitalini hapo.

“Mamlaka ya Bandari wametupatia fedha zaidi ya milioni miambili kukarabaji jengo hili la kituo cha kusafishia damu na wakatupatia vifaa pamoja na viti mwendo vyenye thamani ya milioni, gali la kubebea wagonjwa milioni 150 na gari la kubeba wafanyakazi liligharimu milioni 109 hii inaonyesha namna wadau hawa wanavyoguswa na utoaji huduma hospita ya Temeke hivyo tunawashukuru na waendelee na moyo huo,”amesema.

Amebainisha kuwa tafiti na tathmini zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile Shinikizo la Damu,Sukari,pamoja afya ya akili yamekua yakiongezeka kutokana na ulaji usiofaa ,kutokufanya Mazoezi hivyo niwakati sasa sahihi wananchi kuchagua kufanya Mazoezi na kuacha kula vyakula vyenye chumvi na Sukari Nyingi,pamoja na Matumizi ya Tumbaku au kuendelea.

“Serikali imeanza kutekeleza Afua mbalimbali ili kukabiliana na Magonjwa haya ikiwemo kufanya uratibu jumuishi wa wagonjwa kuanzia kwenye zahati pamoja na kutoa Elimu kwa Wananchi kupitia wataalamu wa Afya ili kusaidia kukabiliana na Magonjwa haya ambayo yamekua tishio kubwa kwa sasa,”amesema.

Awali akitoa taarifa za Utoaji huduma wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke Afisa Muuguzi Mkuu Dkt Joseph Kimaro amesema kuwa Hospitali hiyo tangua kuanzishwa kwake Mwaka 1970 imepata mafanikio Makubwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili kama vile Ufinyu wa eneo la Hospitali hiyo kwa ajili ya kuongeza miundombinu ya utoaji wa huduma kwa Wananchi.

Amesema ongezeko la wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza takwimu zinaonyesha katika hospitali hiyo 2022 /2023 wamehudumia watu 9560 huku 2023/2024 idadi ikiongezeka hadi kufikia 11175 na chanzo kikuu ni ulaji usiofaa.

Hata hivyo amebaisha kuwa wamepata mafanikio makubwa sana kwa sasa wanalaza wagonjwa 250 hadi 300 huku wagonjwa wa nje (OP)zaidi ya 2000 hivyo kituo hiko cha kusafishia Damu wamepata msaada kutoka kwa Mamlaka ya Bandari Nchini ( TPA) ambapo wametoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 200 kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa Jengo pamoja na milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kama vile Viti mwendo pamoja na vifaa vya Kusafishia Damu.

Aidha wito umetoa wito Wadau wengine wajitokeze kutusaidia ili waweze kuboresha huduma za Wananchi na kumuunga Mkono Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye kwa miaka mitatu ya uongozi wake amewekeza fedha kwenye sekta ya Afya na Wananchi wanapata huduma salama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here