Home KITAIFA AMOSI LWIZA MBARONI KUSAMBAZA TAARIFA ZA KUMZUSHIA BINTI ALIYEFANYIWA UKATILI KUWA KAFARIKI

AMOSI LWIZA MBARONI KUSAMBAZA TAARIFA ZA KUMZUSHIA BINTI ALIYEFANYIWA UKATILI KUWA KAFARIKI

Dar es salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata na linamuhoji kwa kina Amos Lutakulemberwa Lwiza mwenye umri wa miaka 54 mkazi wa Kinondoni Tegeta Wazo kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo na uzushi za kifo kumuhusu binti aliyefanyiwa kitendo cha udhalilishaji kupitia mitandao ya kijamii kuwa amekutwa amefariki jambo ambalo si la ukweli.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Agosti 7, 2024 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro amesema baada ya kuona uzushi huo ukisambaa mtandaoni walifuatilia kwa kina na kumbaini mtuhumiwa huyo hivyo amewasihi watu wajiepushe kusambaza taarifa za uongo kwani zimekua zikizusha taharuki ndani ya jamii.

“Ni marufuku kusambaza taarifa ambazo hazina uhakika kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria hivyo nawasihi watu simu walizonazo kujiepusha na kutoa au kuchapisha taarifa za uongo zenye malengo ya kuzusha taharuki katika jamii kwani kufanya hivyo ni Jeshi la Polisi litaendelea kuzingatia maoni ya watu ambayo hayakinzani na sheria za nchi,”amesema SACP Muliro.

Akizungumzia kuhusu hali ya usalama kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Klabu ya Yanga na Simba katika Uwanja wa Benjamini Mkapa SACP Muliro ameeleza kuwa Jeshi siku hiyo limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo.

“Usalama utaimarishwa kwa kiwango cha juu,hivyo tunawakumbusha nimarufuku kwa mtu yeyote kwenda na silaha uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo, watu watakaojihusisha na vitendo vyakihalifu ndani au nje ya uwanja watashughulikiwa haraka kwa mujibu wa sheria,” amesisitiza SACP Muliro.

Mchezo wa soka wa watani wa jadi baina ya klabu ya Yanga na Simba Mtanange huo utachezwa kesho Agoti 8 ,2024 kuanzia saa 1:00 jioni Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here