Home KITAIFA WANANCHI WAJIONEA UTEKELEZAJI MIRADI YA GESI ASILIA NANENANE DODOMA

WANANCHI WAJIONEA UTEKELEZAJI MIRADI YA GESI ASILIA NANENANE DODOMA

📌 Teknolojia ya Uhalisia Pepe yawa kivutio

📌 Elimu Matumizi ya Nishati Safi Kupikia yatolewa

Dodoma

MAONESHO ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma yamekuwa ni sehemu ya wananchi kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Sekta ya Nishati ikiwemo miradi ya Gesi Asilia na Mafuta.

Katika Banda la Wizara ya Nishati wananchi wameonesha kuvutiwa na teknolojia ya Uhalisia
Pepe (Virtual reality) ambayo inawawezesha wananchi kuona moja kwa moja miradi ya uzalishaji, uchakataji na usambazaji wa gesi asilia iliyopo mkoani Mtwara na Lindi.

Kupitia teknolojia hiyo wananchi wameweza kuona namna gesi inavyozalishwa kutoka kwenye visima na kuingiwa kwenye mitambo ya uchakataji kisha kusafirishwa kwa bomba kwenda kwenye matumizi mbalimbali ya viwandani, kuzalisha umeme, kwenye magari, taasisi pamoja na matumizi ya majumbani.

Aidha, Wizara ya Nishati inaendelea kutoa elimu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here