Home KITAIFA TTCL: IMEINGIA MIKATABA NA VYAMA VYA USHIRIKA ZAIDI YA 100.

TTCL: IMEINGIA MIKATABA NA VYAMA VYA USHIRIKA ZAIDI YA 100.

Esther Mnyika, Dodoma

SHIRIKA la Mawasiliano Nchini (TTCL) limesema hadi sasa wameshaingia mikataba na vyama vya ushirika zaidi ya 100 na vyama hivyo vinapatikana kila mkoa nchini.

Akizungumza na leo Agosti, 6 2024 waandishi wa habari Meneja wa Biashara TTCL wa Dodoma Leyla Pongwe kwenye banda la shirika hilo lililopo kkwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayoendelea viwanja vya nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.

Amesema katika maonesho hayo wamewaletea wakulima huduma hiyo ili kuwasaidia kupokea malipo yao kwa haraka na uhakika.

“Wakulima nchini wanatakiwa kujiunga na vyama vya ushirika ili kunufaika na huduma ya malipo ya mkupuo inayotolewa na shirika hili kwa wakulima,” amesema.

“Mwaka huu tumewaletea wakulima malipo kwa mkupuo ambayo yanamuwezesha mkulima kupitia vyama vyao vya ushirika yaani mnunuzi analipa kwa mkupuo kwa vyama alafu vyama vinawalipa wakulima kwa kupitia laini zao za T Pesa,”amesema.

Amesema kwa kufanya hivyo kutamsaidia mkulima kupata masoko makubwa na kufanyabiashara kwa uaminifu kwani sasa TTCL inamkongo hadi nje ya nchi hivyo ni rahisi kupata huduma ya T Pesa.

Pia amesema katika maonesho hayo pia wametoa huduma ya intaneti ya bure kwa wanaotembelea maonesho hayo.

Aidha kauli mbiu ya huduma hiyo inasema’Lipa malipo ya wakulima kwa mkupuo ukiwa na T PESA’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here