Home KITAIFA FCC: WATANZANIA KUTEMBELEA MAONESHO YA KILIMO NA UFUGAJI ILI KUONGEZA UZALISHAJI

FCC: WATANZANIA KUTEMBELEA MAONESHO YA KILIMO NA UFUGAJI ILI KUONGEZA UZALISHAJI

Na Esther Mnyika, Dodoma

TUME ya Ushindani Nchini (FCC),William Erio imetoa wito kwa watanzania kutembelea maonesho ya Kilimo ili kujua mambo yanayohusu kilimo na ufugaji kuongeza uzalishaji wenye bidhaa zenye ubora na kupata soko zuri ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa leo Agosti,5 2024 na Mkurugenzi Mkuu FCC, Wiliam Erio kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa sheria ya ushindani Namba 8 ya mwaka 2003 kifungu cha 36 na kanuni za mikataba ya watumiaji za mwaka 2014 zinawataka wauzaji na watoa huduma wote wanaotumia mikataba ya watumiaji kuleta mikataba yao FCC kwaajili ya mapitio na usajili.

“Sisi tumeshiriki katika maonesho haya kwaajili ya kutoa elimu kwa umma ili wajue shughuli zinazofanywa na FCC jukumu letu kubwa ni kuhakikisha kulinda na kushajiisha ushindani kwa sababu wapo baadhi ya watu wana biashara zinafanana hivyo ni vizuri kuwapa elimu,”amesema.

Amesema masuala mengine yanasimamiwa na taasisi zingine FCC wanafanya kwa upande wa bei na kuzuia mienendo hadaifu na kandamizi inaweza ikamkwamisha mlaji.

Amesema wamekuja kuwapa elimu kuhusu kushajihisha ushindani na kuwaeleza na masuala ya msingi ya jinsi ya kumlinda mlaji na kuepukana na bidhaa bandia na madhara yake.

“Kwasababu wenyewe katika uzalishaji wanaweza kuagiza bidhaa wanazotumia katika uzalishaji bidhaa hizi kama zitakuwa bandia zitafanya bidhaa zao kukosa ubora ulio kusudiwa,”amesema.

Ameongeza kuwa wakati mwingine hata kiwango cha uzalishaji kuwa kidogo kutokana na bidhaa bandia kuliko kingeweza kupatikana.

Aidha amesema kwenye kilimo kuna mambo kama pembejeo wanazotumia wakipata pembejeo sahihi wanazalisha kiwango kikubwa cha mazo kwa mda mfupi na pembejeo ikiwa bandia au za kugushi lengo hilo linaweza lisifanikiwe.

Erio amesema kuwafundisha namna gani ya kuepukana na bidhaa bandia ikiwa na pamoja kununua bidhaa zao kutoka kwa wazalishaji wenyewe au watu walioidhinishwa na wazalishaji ili wapate vitu ambavyo vitawasaidia katika kuwa na bidhaa bora.

Kaulimbiu ya maonesho hayo “Tuchague viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, uvuvi na mifugo”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here