Na Esther Mnyika, Dodoma
TUME ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imesema kutungwa kwa sheria ya umwagiliaji ni kuondoa changamoto zilizokuwa zinazoikabili sekta ya umwagiliaji nchini.
Akizungumza leo Agosti 5,2024 kwenye maonesho ya Kimataifa ya kiimo yanayoendelea kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma Afisa Sheria mwandamizi NIRC, Amina Mweta amesema ushiriki mdogo wa wakulima na sekta binafsi katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ni chanzo cha uanzishwaji wa sheria hiyo.
Ameeleza kuwa kutokana na hali iliyokuwepo ya changamoto ambazo zimeikabili sekta ya umwagiliaji sheria imesaidia kuongezeka kwa mchango wa umwagiliaji katika uzalishaji wa chakula na lishe na kuongezeka kwa pato la wakulima na Taifa kwa ujumla.
“Sheria ya Taifa ya umwagiliaji na.4 ya mwaka 2013 imetugwa na kupitishwa na bunge mwaka 2013 ikatiwa saini na Rais DktSamia Suluhu Hassan octaba 20,2013 sheria hii imeanzishwa na tume ya umwagiliaji ili kusimamia kilimo cha umwagiliaji na kutatua changamoto za wakulima,”mesema.
Ameongeza kuwa sababu nyingine imesema kuanzishwa kwa sheria ya umwagiliaji ni pamoja ni udhaifu wa mifumo ya kitaasisi ambao ulikua haukidhi kasi ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na uvamizi wa maeneo ya ardhi yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Pia amebainisha vitendo vilivyokatazwa katika sheria ambapo ni pamoja na kuingia katika ardhi ya umwagiliaji kwa madhumini tofauti na umwagiliaji.
Aidha amesema kuruhusu sumu ya viwandani au uchafu wa majumbani kuingia kwenye skimu yeyote ya umwagiliaji bila kutibu maji kikamilifu.
Kwa upande wake Mhandisi Mwandamizi wa Umwagiliaji wa NIRC, Naomi Mcharo amesema kwa mwaka huu wa fedha NIRC wamejipanga kuchimba visima 1000 nchi nzima.
Amesema NIRC wanaendelea na miradi mbalimbali ya umwagiliaji nchini ili kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinakuwa na kumnufaisha mkulima.