Home KITAIFA VETA IMEKUJA NA TEKNOLOJIA AMBAZO ZITAFANYA KILIMO KUKUA NCHINI

VETA IMEKUJA NA TEKNOLOJIA AMBAZO ZITAFANYA KILIMO KUKUA NCHINI

Esther Mnyika, Dodoma

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema kwenye Maonesho ya Kilimo ya Nanenane mwaka huu imekuja na teknolojia ambazo zitafanya kilimo kukua nchini kutokana kwa kupata mashine za gharama nafuu kupatikana.

Hayo ameyasema leo Agosti, 4 2024 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, CPA Anthony Kasore wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Banda la VETA kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

“VETA kuwa imejipanga katika kuhakikisha Wakulima nchini wanalima Kilimo chenye tija kutokana na teknolojia mbalimbali zilizobuniwa na vyuo vya VETA,” amesema.

Amesema kuwa vijana na wananchi watumie vyuo hivyo wananchi na vijana kutumia fursa katika kupata ujuzi na kuweza kujiajiri.

CPA Kasore amrongeza kuwa vyuo vya 80 vimeshajengwa katika Mikoa na Wilaya huku vyuo 65 vipya vinajengwa katika Wilaya na kufanya kila Wilaya kuwa na Chuo cha Ufundi Stadi.

Amesema vyuo amesema kuwa katika maonesho hayo wamekuja na mashine ya kutengeneza udongo kwa ajili ya kuoteshea mazao ya bustani ambapo udongo wa kuoteshea ulikuwa umatoka nje ya nchi kwa gharama kubwa ukilinganisha na mashine iliyopo VETA ya gharama nafuu.

Kasore amesema VETA imegusa fani katika kila Chuo kuendana na mazingira yake lengo ikiwa ni kufanya mhitimu kutafuta soko lake bila kukabiliwa na changamoto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here