Home KITAIFA TANESCO YAWAOMBA WANANCHI NA WAKULIMA KUJITOKEZA KWENYE BANDA LAO ILI KUPATA ELIMU

TANESCO YAWAOMBA WANANCHI NA WAKULIMA KUJITOKEZA KWENYE BANDA LAO ILI KUPATA ELIMU

Dodoma

SHIRIKA la umeme Nchini (TANESCO) limetoa rai kwa wananchi na wakulima waliopo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane kujitokeza kwenye banda lao ili kupata elimu ya namna bora ya matumizi ya umeme katika shughuli zao za kila siku.

Akizungumza leo Agosti 4,2024 katika viwanja vya maonesho vya nanenane vilivyopo Nzuguni jijini Dodoma Meneja Masoko wa TANESCO, Silvester Matiku amesema wameshiriki katika maonesho hayo wakiwa kama taasisi muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi katika sekta ya kilimo.

Amesema wanaendelea na maboresho ya mita za Luku na zoezi hilo wanatarajia kulikamilisha mwezi wa 11 mwaka huu hivyo amewataka wananchi kuhakikisha wanafanyia marekebisho mita zao ili waendelee kutumia huduma bora zinazotolewa na shirikia hilo.

“Wananchi wanapaswa kujitokeza hapa ili waje kujifunza namna shirika lilivyojipanga kuwahudumia lakini namna nzuri ya matumizi ya umeme na miradi iliyopo ukiwemo wa bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo limekamilika kwa asilimia 98.33”,Amesema Matiku.

Amesema kutumia kuboreshwa kwa teknolojia kumesaidia kupunguza matumizi ya umeme kwani sasa hivi vifaa vya kutumia umeme vimeboreshwa zikiwemo balbu zinazotumia umeme kidogo.

“Tunaomba wananchi waje kwa wingi wajifunze pia na ya kujilinda(usalama) wakati wa kutumia umeme lakini poa wajue jinsi ya kujihudumia wakiwa popote oindi wanapopata changamoto lakini hata wakitika kuunganishiwa umeme.

Tuna umeme wa kutosha nchini na lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma hiyo hivyo nitoe rai kwa wananchi pindi wanapoona umeme umeshawafikia kwenye maeneo yao wachangamkie fursa kwani serikali inataka kila mwananchi afikiwe na huduma hiyo kwa ustawi wa uchumi wa Taifa,”amesema.

Amesema serikali inawekeza kwenye uzalishaji wa umeme ili uwe wakutosha nchini lakini pia hata kuuza nchi jirani ili pia kuchochea ukuaji wa uchumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here