Home KITAIFA BAADA YA HANIYE , KAMANDA MWINGINE WA HAMAS ADAIWA KUUAWA NA ISRAEL

BAADA YA HANIYE , KAMANDA MWINGINE WA HAMAS ADAIWA KUUAWA NA ISRAEL

SHAMBULIO la anga la Israel limeelezwa kuua watu 5 katika Ukingo wa Magharibi, akiwemo kamanda wa Hamas.

Shambulizi la anga la Israel dhidi ya gari katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu limetajwa kumuua kamanda wa kundi la wapiganaji la Palestina Hamas siku ya Jumamosi kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Hamas.

Shirika la habari la Palestina WAFA likirejea ripoti ya maafisa wa afya limesema wanaume wengine wanne pia waliuawa huku likisema kuwa utambulisho wao haukuwa wazi.

Jeshi la Israel limesema lilifanya shambulizi la anga dhidi ya wanamgambo karibu na mji wa Tulkarm, Ukingo wa Magharibi.

Vyombo vya habari vya Hamas vimesema gari lililokuwa limebeba wapiganaji lilishambuliwa na kwamba mmoja wa makamanda wa brigedi zake za Tulkarm aliuawa.

Ghasia katika Ukingo wa Magharibi tayari zilikuwepo kabla hata ya vita vya Israel na Hamas huko Gaza vilivyoanza tarehe 7 Oktoba 2924 na imeongezeka tangu wakati huo huku uvamizi wa mara kwa mara wa Israel katika eneo hilo, ambalo ni kati ya yale ambayo Wapalestina wanatafuta taifa ukipamba moto.

Mvutano wa eneo zima umeongezeka wiki hii baada ya mauaji ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh huko Tehran siku ya Jumatano, siku moja baada ya shambulio la Israeli huko Beirut kumuua kamanda mkuu wa jeshi la Hezbollah Fuad Shukr.

Kifo cha Haniyeh kilikuwa ni miongoni mwa mfululizo wa mauaji ya viongozi wakuu wa Hamas huku vita vya Gaza kati ya wanamgambo wa Palestina na Israel vikikaribia mwezi wa 11 na wasiwasi wa mzozo huo kuenea katika eneo lote la Mashariki ya Kati ukiongezeka.

Hamas na Iran wote wameishutumu Israel kwa kutekeleza mauaji hayo na wameahidi kulipiza kisasi dhidi ya adui wao.

Israel haijakubali wala kukana kuhusika na kifo hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here