Home KITAIFA DK.MARY AMEWATAKA WAKULIMA NCHINI KUTUMIA MBEGU ZENYE VIWANGO.

DK.MARY AMEWATAKA WAKULIMA NCHINI KUTUMIA MBEGU ZENYE VIWANGO.

Dodoma

MKURUGENZI wa Kampuni ya Namburi Agricultural Company ni wazalishaji wa mbegu bora Dk. Mary Mgonja amewataka wakulima nchini kutumia mbegu zinazozalishwa nchini ambazo zinaviwango na zinahimili ardhi aina zote.

Akizungumza leo Agosti, 2 2024 na waandishi wa Habari Dk. Mary kwenye maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nanenane Mkoani Dodoma amesema kampuni yao imekuwa ikizalisha mbegu zenye ubora lakini pia zinahimili mpaka kwenye ukame.

“Hapo sisi tunambegu mpaka zinazohimili kwenye ukame mbapo mkulima wa maeneo hayo anaweza kuzitumia na akafanikiwa kuvuna vizuri na kufanyabiashara,”amesema Dk. Mgonja.

Aidha ameipongeza Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu Bora Nchini (TOSCI) kwa kuitangaza nchi lakini pia kuzuia uuzaji wa mbegu bandio.

“Nitoe rai kwa wakulima pia kuwa makini wakati wa kununua mbegu kuhakikisha mbegu hizo zina alama ya Tosci,”amesema.

Ameongeza kuwa kampuni ya Mamburi inafanya shughuli zake za uchakataji na uzalishaji katika mkoa wa Songwe lakini wanasambaza mbegu zao kwenye maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha kila mkulima anapata mbegu hizo.

Dk. Mgonja amewata wastaafu kutumia muda huo wa kuingia kwenye kilimo ili kuendelea kufanyakazi na kujiimarisha kiafya na kiuchumi pia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here