Home KITAIFA TUMEWAFIKIA KISIWA CHA CHOLE UMEME UNAKUJA

TUMEWAFIKIA KISIWA CHA CHOLE UMEME UNAKUJA

Pwani

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea na utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme kwenye kisiwa cha chole kilichopo Wilayani Mafia Mkoani Pwani.

Mradi huu unahusisha kuvusha umeme kupitia baharini kwa kutumia waya wa marine cable wenye urefu wa zaidi ya kilomita moja na nusu.

Upatikanaji wa umeme wa uhakika ilikuwa ndoto ya siku nyingi kwa wakazi wa kisiwa cha chole, na utekelezaji wa mradi huu unaenda kubadilisha
Kabisa historia ya muda mrefu ya kisiwa hicho ambacho hakikuwahi kuwa na huduma ya umeme.

Hizo zikiwa kati ya juhudi za Serikali chini ya uongozi thabiti wa Rais.Samia Suluhu Hassaĺn Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Nishati inayosimamiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma ya umeme wa uhakika na wa kutosha ili kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here