Home KITAIFA RAIS DK. MWINYI KUSHIRIKI UZINDUZI WA SGR.

RAIS DK. MWINYI KUSHIRIKI UZINDUZI WA SGR.

Na Mwandishi wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi atashiriki Uzinduzi wa Usafiri wa Treni ya Umeme kwa kutumia Reli ya Kisasa (SGR).

Uzinduzi wa mradi wa SGR utafanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kusafiri na treni hiyo safari yenye umbali wa kilomita zaidi ya 400 ambayo inatarajiwa kuanza jijini Dar es Salaam Agosti, 1 2024.

Vilevile Rais Dk. Mwinyi atashiriki uzinduzi huo kwa kupanda treni hiyo kuelekea Dodoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here