Home KITAIFA RAIS DK.SAMIA AONGOZA MKUTANO WA 15 WA TNBC

RAIS DK.SAMIA AONGOZA MKUTANO WA 15 WA TNBC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akiongoza Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Julai, 29 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) akizungumza kabla ya kufungua Mkutano wa 15 wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai,29 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania M Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) akitoa Tuzo kwa Mikoa mitatu iliyofanya vizuri kwenye majadiliano na kuchangia Ukuaji wa Uchumi. Mikoa hiyo ni Dodoma, Dar es Salaam na Kilimanjaro katika Mkutano huo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Julai,29 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Heshima Pro Business Environment Award kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai, 29 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam Julai,29 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here