Home AFYA ASILIMIA 50 YA WATUMISHI WANAHITAJIKA MIKOA YA PEMBEZONI

ASILIMIA 50 YA WATUMISHI WANAHITAJIKA MIKOA YA PEMBEZONI

Dar es Salaam

WATUMISHI wa Afya nchini wametakiwa kwenda kufanya kazi katika Halmashauri za pembezoni mwa nchi ili kupunguza uhaba wa wataalamu hao unaokadiriwa kuwa ni zaidi ya asilimia 50.

Upungufu huo unaovikabili vituo vya Afya, Zahanati na baadhi ya Hospitali za Halmashauri umechangia kudhoofisha hali ya utoaji wa hudumaza Afya.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hayo leo Julai 29, 2024 wakati wa Kongamano la kumbukizi la Rais Mstaafu Benjamini Mkapa lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaa.

“Niwatoe hofu watumishi wa Afya kutoogopa kufanya kazi katika maeneo ya pembezoni mwa nchi kwa kuwa huduma zote muhimu za kijamii zinapatikana ikiwemo umeme, barabara, maji pamoja na shule,” amesema Waziri Ummy.

Amesema, leo mkutano huo utajadili masuala ya rasilimali watu kwenye Sekta ya Afya ambao ni uzalishaji wa wataalamu wa Afya ndani ya nchi, ubora wa watumishi wa Afya kwa kuhakikisha watumishi wanasalia kwenye maeneo waliyopangiwa kuhudumia wananchi.

Waziri Ummy amesema Hayati Rais Benjamini Mkapa alikua ni muumini na kinara waliofanya kazi kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za Afya ikiwemo Sheria ya Bima ya Afya ya NHIF aliyoiasisi Mwaka 2,000.

Amesema, hivi sasa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) umekua ndio chanzo kikuu cha mapato yanayotokana na huduma zinazotolewa kupitia mfuko huo.

Kongamano hilo linakutanisha wadau mbalimbali katika Sekta ya Afya ambapo watajadili masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya ambapo linatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Julai 30, 2024 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Tunategemea kupata maoni na ushauri wa wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya ikiwemo Sekta binafsi katika kutengeneza mkakati wa Sita wa Taifa wa Sekta ya Afya Mwaka 2026/2031 ambao inaendana na kukamilisha kwa dira ya Taifa ya Mwaka 2050,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here