Home KITAIFA KAMPUNI ZA UWEKEZAJI KATIKA UJENZI CHINA ZATEMBELEA MOI

KAMPUNI ZA UWEKEZAJI KATIKA UJENZI CHINA ZATEMBELEA MOI

Na Abdallah Nassoro-MOI

TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), leo Julai 24, 2024 imepokea ujumbe kutoka makampuni ya uwekazaji kwenye sekta ya ujenzi wa majengo kutoka China walioonesha nia ya kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi ya taasisi hiyo.

Timu hiyo ya wataalam imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dk. Lemeri Mchome ambaye amewaeleza uwepo wa miradi mikubwa miwili ya ujenzi ya kituo cha matibabu ya mgongo na utengamao Mbweni na kituo cha umahiri cha tiba ya ubongo na mishipa ya fahamu Mloganzila.

“Tunao mradi wa ujenzi wa kituo cha matibabu ya mgongo na utengamao Mbweni mpiji jijini Dar es Salaam, mradi huu utakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 160, gharama za ujenzi wa mradi huu zinakadriwa kufikia 164.4 bilioni” amesema Dk. Mchome na kuongeza

“Mradi mwingine ni wa ujenzi wa kituo cha umahiri wa tiba ya ubongo na mishipa ya fahamu wenye uwezo wa kulaza wagonjwa 600, mradi huu utatekelezwa Mloganzila…ujio wenu kwetu ni muhimu kuona kama tunaweza kushirikiana katika utekelezaji wa miradi hiyo,”

Kiongozi wa timu hiyo Naibu Meya wa mji wa Taian nchini China, Tan Chuon Ping amesema lengo la ziara hiyo ni kuibua fursa za uwekezaji na ushirikiano katika miradi ya ujenzi wa majengo baina yao na MOI.

“Makampuni yetu yana uzoefu mkubwa katika sekta ya ujenzi, pia tuna uzoefu wa uendeshaji wa hospitali, hivyo kwetu hii ni fursa ambayo tungependa kushirikiana nanyi katika kuutekeleza”amesema Ping

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here