Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wasanii kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii.

Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Mwanamuziki kizazi kipya Omary Ally Mwanga maarufu Marioo , Ikulu Zanzibar Julai,22 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amempongeza Marioo kwa kazi nzuri ya kuitangaza Tanzania kupitia kazi yake ya muziki.

Naye Marioo ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa fursa aliyoipata ya kurekodi wimbo wake mpya wa Hakuna Matata katika mazingira ya vivutio vya Zanzibar .
Pia amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa jitihada zake kubwa za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.
