Home AFYA MUHIMBILI YAPEWA TUZO YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI

MUHIMBILI YAPEWA TUZO YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI

Dar es Salaam

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea tuzo inayotambua mchango wake katika kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya nchini ambayo imetolewa na Mamlaka ya Kupambana Madawa ya Kulevya (DCEA).

Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mohamed Janabi amesema hospitali hiyo ilianzisha kliniki ya Methadhone mwaka 2011 ikiwa ni ya kwanza nchini ili kutoa huduma kwa warahibu wa dawa ya kulevya aina ya afyuni waweze kuondokana na tatizo hilo.

Profesa Janabi amesema tangu kuanzishwa huduma hiyo hadi kufikia Juni 2024 jumla ya warahibu 3,840 wameandikishwa kupata huduma ya methadone wanaume wakiwa 3,692 na wanawake 148 ambapo warahibu 900 wanaohudumiwa kila siku kunywa dawa ya methadone kati yao wanawake ni 30.

MNH imewapa ajira warahibu 58 ambao wamepata nafuu ya kubadilika tabia na kuacha kabisa kutumia madawa ya kulevya ambao sasa wanafanya shughuli mbalimbali kama vibarua ikiwa ni sehemu ya tiba kazi, 10 wanasukuma viti mwendo, 33 wanahudumia bustani, wawili huduma kwa wateja na 13 wapo kitengo cha utasishaji.

Kwa upande wake Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana Madawa ya Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema mamlaka hiyo inathamini na kutambua mchango na ushirikiano unaotolewa na MNH na wadau wengine ili kuhakikisha biashara na matumizi ya madawa ya kulevya vinakomshwa nchini

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here