Home KITAIFA HALMASHAURI WEKENI MIKAKATI YA KUTOKOMEZA MALARIA

HALMASHAURI WEKENI MIKAKATI YA KUTOKOMEZA MALARIA

Pwani

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo amezishauri halmashauri zote nchini kuweka mkakati wa kununuaa dawa za viluwiluwi inayozalishwa na kiwanda cha TBPL kilichopo Kibaha Mkoani Pwani ili kuuwa mazalia ya mbu na kusaidia kutokomeza kabisa ugonjwa wa malaria ambao umekuwa tishio kwa kupelekea watu kupoteza maisha.

Ushauri huo ameutoa leo Julai 16 na Dk. Jafo Mkoani Pwani katika ziara yake alipotembelea kiwanda hicho ambapo amesema bado changamoto ya ugonjwa wa Malaria nchini ni kubwa na fedha nyingi zimekuwa zikitumika kutibu malaria wakati uwekezaji mkubwa umefanywa kujenga kiwanda cha kuzalisha dawa hiyo ya kutokomeza kabisa ambapo miundombinu yake iliyogharimu bilioni 52 cha kushangaza nchi jirani ndiyo zinazokuja kununua dawa hizo.

“Bado tuna tatizo la malaria kiwanda hiki kipo Tanzania na ni cha pekee Barani Afrika lakini bado hatujaona thamani hasa bidhaa ya matumizi ya kinachozalishwa leo haiwezekani Kenya Angola,Nigeria Mozambique na Zanzibari wanakuja kuchukua dawa hii hapa kwetu wakatokomeze malaria kwao lakini sisi tumejikita katika tiba kutumia fedha nyingi kuagiza dawa badala ya kinga,” amesema Waziri Jafo.

Ameliagiza Shirika la Maendeleo (NDC ) kufanya kampeni au kipiga debe dawa hiyo kupitia vikundi mbalimbali mikutano ya Alati ambayo wanakuwepo viongozi wote wa halmashauri zote nchini wao kwenda na ajenda ya kutangaza dawa hiyo ya kuua viluwiluwi vya mbu ili kusaidi kutokomeza malaria na kufikia Zero kama Zanzibari wamefanikiwa na hapa inawezekana.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo NDC Dk. Nicolaus Shombe amesema uwezo wa kiwanda uzalishaji wake ni mzuri na wataalamu wake wakati kinajengwa lengo lake kuu lilikuwa kuhakikisha wanapambana na malaria ifikapo 2030 Malaria inakuwa 0 na serikali ndiyo iliyokusudiwa iwe inanunua dawa hizo na walinunua kidogo baadae ikabakia na wanauza bidhaa hiyo katika nchi jirani 6 ikiwemo Botswana,Angola,Mozambique, Nigeria, na kwa asasi mbalimbali za kiraia ikiwemo zinazoshughulika na mazingira ya wakimbizi

“Hii bidhaa ni ya kijamii kama ikinyunhiziwa majumbani sehemu ambazo mazalia ya mbu yanakuwepo lakini nyumba nyingine hazijanyunyizia mbu wanahamahama na zoezi halitafanikiwa hivyo ni vyemaa jitihada ikafanywa nchi nzima ndiyo mafanikio yataonekana kama ilivyokuwa Zanzibari,” amesema Dk. Shombe

Hata hivyo Kiwanda hiko kinazalisha bidjaa mbalimbali ikiwemo mbolea za mazao, chanjo za wanyama na dawa za viluwiluwi

Katika hatua nyingine Waziri Jafo amefanya ziara yake katika viwanda vilivyopo mkoani Pwani Kongani za viwanda Modern industrial Park pia kiwanda cha Sino tan ambapo alifanya mazungumzo nao na kuahidi kuwa atazungumza na Shirika la Reli Nchini (TRC) kujenga kituo cha treni maeneo hayo ya kiwanda cha Sino tan ili kusidia kuwarahisishia usafiri wanaposafirisha bidhaa watakazozalisha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here