Matukio mbalimbali Mkoani Rukwa ambapo wananchi wamejikusanya kumshuhudia Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye Julai,16 2024 anatarajiwa kuzindua vihenge na maghala ya kisasa ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), katika eneo la Kanondo, Mkoani Rukwa.
Kukamilika kwa Mradi huo kumewezesha NFRA kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka za aina tofauti kama vile mahindi, mtama na mpunga katika Mkoa wa Rukwa kutoka tani 33,500 hadi tani 58,500; kwa maana ya ongezeko la vihenge tani 20,000 na maghala tani 5,000.
Maghala hayo ya kisasa yana mfumo mzuri wa kupitisha hewa ambao pia unaoruhusu ufanisi katika uhudumiaji mazao (improved ventilation sytem and improved logistical system); ikiwa ni pamoja na utumiaji wa zana mbalimbali za kazi (matrekta, mizani, elevators).
Mradi huo ulianza Julai 2019 na umegharimu Dola za Marekani milioni 6,019,000 sawa na shilingi bilioni 14. NFRA inaendelea kujipanga kuongeza uwezo wa teknolojia ya vihenge na maghala ili kuendana na uzalishaji wa chakula hapa nchini.