Home MICHEZO WAZIRI MKUU AZINDUA MITAMBO YA KISASA YA KURUSHIA MATANGAZO

WAZIRI MKUU AZINDUA MITAMBO YA KISASA YA KURUSHIA MATANGAZO

Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 15, 2024 amekagua na kuzindua mitambo na vifaa vipya vya kurushia matangazo vya kampuni ya Azam Media Limited.

Vifaa hivyo ni pamoja na Magari ya kisasa ya kurushia matangazo (OB Van), kamera za kisasa pamoja na mfumo wa kusaidia maamuzi viwanjani (VAR).

Vifaa hivyo vilivyogharimu shilingi bilioni tano vitatumika katika kurushia matangazo ya mpira wa miguu wa ligi Kuu Tanzania bara na Zanzibar pamoja michezo mingine.

Akizungumza na wafanyakazi wa Azam Media pamoja na wadau wa michezo Majaliwa amesema manunuzi ya vifaa hivyo ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwani kunaifanya Tanzania kuwa nchi ya kipekee kuwa na vifaa vya kisasa vya aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Majaliwa pia ameshuhudia uzinduzi wa chaneli mpya ya Azam 4 HD ambayo itatumika kurusha ligi kuu ya Ufaransa (Legue 1) na ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here