Home KITAIFA DK. SAMIA: BEI YA MAHINDI KUUZWA KWA SHILINGI MIA 600 KWA KILO...

DK. SAMIA: BEI YA MAHINDI KUUZWA KWA SHILINGI MIA 600 KWA KILO MOJA

Katavi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan akihitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Katavi Julai 15 2024 ambapo wananchi wa Mpimbwe waliambiwa kuwa bei ya mahindi vijijini itaanzia kuuzwa kwa shilingi mia 600 kwa kilo moja na mjini kwa shilingi mia 650.

Ambapo Vituo vya vijijini vya Wakala wa Hifadhi ya Chakula( NFRA) kununua kwa bei ya mahindi kwa shilingi mia 600 na mjini shilingi mia 650 ambapo bei ya awali ilikuwa shilingi mia 500 kwa kilo moja.

Rais Dk. Samia amekuwa mkoani Katavi kwa siku tatu ambapo pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, alizindua pia vihenge na maghala ya kisasa ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), na kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka za aina tofauti kutoka tani 5,000 hadi tani 28,000.

Naye Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameshirikisha katika ziara hiyo amemshukuru Rais Dk.Samia kwa niaba ya wakulima amesema kuwa mbolea ya ruzuku itaendelea kuwepo kwa maelekezo ya Rais 2025 hadi 2026.

Ameongeza kuwa Septemba mwaka huu wanatarajia kutangaza bei elekezi ya mbegu na serikali itasimamie bei elekezi hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here