Home KITAIFA TTCL INATARAJIA KUFIKISHA HUDUMA ZAKE DRC.

TTCL INATARAJIA KUFIKISHA HUDUMA ZAKE DRC.

Leah Choma, Dar es Salaam

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema linaendelea mchakato wa kufikisha huduma zake nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ikiwa ni muendelezo wa kupeleka huduma hiyo kwa nchi za jirani.

Akizungumza leo Julai 12. jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 48 kimataifa ya Biashara mkama Sa,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya TTCL (T-pesa),Lulu Mkudde wakati akiongea na waandishi wa habari,amesema Ambapo mpaka sasa huduma hiyo imefikishwa katika nchi nne ikiwemo Burundi,Rwanda,Zambia na Malawi.

“Tunaposema tunafungua milango ya kidigitali inamaanisha kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi katika kutumia huduma za Interneti katika kutekeleza huduma mbalimbali kwa watu wengine,”amesema na kuongeza

Hadi sasa shirika limefanya mambo mbalimbali ikiwemo huduma ya TTCL – Pesa ambapo katika Sabasaba wqmekuja na huduma ya Akaunti Pepe inamuwezesha mteja kufungua akaunti yake bila hitaji ,mteja anauwezo wa kutumia akaunti yako masaa 24 kwa siku.

Amesema sasa,Shirika limesambaza Mkongo wa Taifa katika mikoa yote nchini ambapo zaidi ya wilaya 98 zikiwa nazo zimefikishiwa Mkongo wa mawasiliano.

Mkudde amesema juhudi hizo zote zinalenga kuhakikisha juhudi za huduma za Elimu, Afya na Maendeleo ya kiuchumi ambayo yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini.

“Niwahakikishie TTCL ,itahakikisha huduma za mawasiliano inakuwa nzuri ili kuwapa fursa wananchi kupata huduma mbalimbali za kujipatia shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato kupitia fursa hii ya Interneti kwa gharama nafuu,”amesema

Akizungumzia Huduma ya T-cafe,Mkudde amesema huduma ya T -Café ni huduma ya WiFi ambayo ina waondolea adha wafanyabiashara, waandishi wa habari na wataalamu wa masuala ya ushauri katika kufanya kazi zqo wakiwa nje ya ofisi.

Amesema ni huduma ambayo inasaidia mtu yoyote kufanya kazi nje ya ofisi kwa kupata uwezo wa kutumia huduma zao katika kutekeleza huduma zake .

“Shirika limeanzisha huduma hii ili kuwawezesha wateja wote kufanya shughuli zao kwa haraka na gharama nafuu,ambapo kwa kipindi hiki cha Sabasaba tumeshuhudia huduma hii inavyofanya kazi kwa speedi ya hali ya juu na wananchi kwa wakati wote walikuwa wakitumia katika maonesho hayo,”amesema.

Aidha amesema kupitia maonesho haya,TTCL imepata fursa ya kutoa elimu na kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu huduma hiyo wanayoitoa ambayo inamfikia mwananchi moja kwa moja .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here