Home KITAIFA WANAWAKE GOMBEENI NAFASI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

WANAWAKE GOMBEENI NAFASI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Tabora

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda (MCC) amewahimiza wanawake wenye uwezo na sifa za uongozi kujitokeza kugombea nafasi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Chatanda ameyasema hayo Julai 11 2024 katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika Kata ya Ibelamilundi Wilaya ya Uyui na Kata ya Ifucha Wilaya ya Tabora Mjini.

“Ninawaomba wanawake wenye uwezo na sifa zinazotakiwa, jitokezeni kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu,”amesisitiza.

Aidha, Chatanda amewataka wanawake kujiandikisha kwa wingi katika daftari la kudumu la mpiga kura.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here