Home KITAIFA MHANDISI SANGWENI:WANANCHI WANAPASWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

MHANDISI SANGWENI:WANANCHI WANAPASWA KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Na Esther Mnyika, Lajiji Digital

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli Nchini (PURA),Mhandisi Charles Sangweni amesema kutokana na ugunduzi wa gesi unaoendelea nchini wananchi wanapaswa kutumia  nishati safi ya kupikia.   

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli Nchini (PURA) Mhandisi Charles Sangweni

Akizungumza leo Julai 12 2024 Mhandisi Sangweni waandishi wa habari leo Julai 12,2024 wakati alipotembelea katika banda la mamlaka hiyo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) amesema wapo mbioni kutangaza vitalu vipya vya uchimbaji mafuta na gesi katika Ukanda wa Pwani hivi karibuni.

Amesema  wanafanya  tunafanya tafiti mbalimbali za kuwezesha jambo hilo liwezekane kwakuzalisha kiasi cha gesi ambacho kitaweza kuhudumia majumbani,katika magari na kwenye maeneo mengine.

“Tumeweka malengo yakutumia nishati safi yakupikia kufikia asilimia 80 mwaka 2034 lazima,tutoke kwanye matumizi ya nishati ambayo inachafua hali ya hewa kama mikaa na kuni  twende tukatumia nishati ambayo haina madhara kwa kiasi kikubwa,”amesema  Mhandisi Sangweni.

Amesema hadi sasa kuna maeneo ambayo tayari yameshagunduliwa gesi ikiwemo Mnazi Bay pamoja na Songosongo iliyopo Mtwara.

Amesema wamefanya utafiti katika maeneo tofauti nchini na kuwa asilimia 50 ya eneo lote nchini kuna miamba tabaka yenye mafuta na katika maeneo hayo mengi yako Ukanda wa Pwani,Kati na Nyanda za Juu maeneo ya Mbeya.

“PURA iko mbioni kutangaza maeneo mapya ya uwekezaji nchini kwenye vitalu vya mafuta na gesi na tunashirikiana na wenzetu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),” amesema Sangweni.

Sangweni amesema katika maonesho hayo wameendelea kuwa elimisha wananchi na washiriki kuhusu kazi na fursa zilizopo kwenye mkondo wa juu wa petroli nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here