Home KITAIFA PURA YAJIPANGA KUONGEZA UWEKEZAJI

PURA YAJIPANGA KUONGEZA UWEKEZAJI

Na Esther Mnyika,@ Lajiji Digital

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema itahakikisha inaongeza wawekezaji kwenye maeneo ambayo yako wazi ikwa lengo la kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani na majumbani.

Akizungumza leo Julai 11 2024 na waandishi wa habari alipotembelea kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kitaifa ya Dar es Salaam (DITF) Mwenyekiti wa bodi ya Wakurungezi PURA, Halfani Halfani alisema PURA ina majukumu ya kusimamia na kudhibiti shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli.

Amesema jukumu la PURA kifungu Na 12 cha Sheria ya Petroli 2015 ni kumshauri Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Petroli juu ya mambo yanayohusu mkondo wa juu wa Petroli nchini.

“PURA tunajukumu la kusimamia shughuli zote za mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika kwa ajili ya soko la nje ya nchi,”amsema Halfan.

Amesema kwa muda mrefu wamekuwa hawana wawekezaji wa kutosha hivyo watahakikisha inaongeza wawekezaji hao katika maeneo ambayo yapo wazi.

Halfan ametaja mafanikio yaliopatikana kwenye gesi asilia kuwa ni pamoja na kuchagia Kwa wastani wa asilimia 50 ya Umeme unaozalishwa nchini, kuongeza matumizi ya gesi asilia viwandani, kupitia majumbani, na kwenye magari.

Amesema Watanzania zaidi ya 1,428 wamepata ajira za kudumu na za muda katika miradi ya ufatiliaji wa uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini

“Kuanzishwa Kwa kazidata ya watoa huduma wa kitanzania ambapo kampuni za watu zaidi ya watu 2000 wamesajiliwa,” amesema.

“Kuanzishwa Kwa kazidata ya watoa huduma wa kitanzania ambapo kampuni za watu zaidi ya watu 2000 wamesajiliwa”. alisema.

Akizungumzia maonesho hayo Kwa kusema awali yalikuwa kama gulio lakini kwa sasa yameboreshwa na kuwa na hadhi ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa kusimamia na kuyawezesha na kuwa na hadhi ya kimataifa.

Amewataka wawekezaji wenye uwezo kuwekeza nchini wafike kwa sababu Tanzania ni sehemu salama pa biashara na uwekezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here