Home KITAIFA CHATANDA AWASILI MKOANI TABORA

CHATANDA AWASILI MKOANI TABORA

TABORA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda (MCC) amewasili Tabora Kwa ajili ya Ziara,akiambatana na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Suzan Kunambi (MNEC),Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji na Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa.

Ziara hiyo ya Viongozi hao inalenga kuhamasisha wananchi,wanachama wa CCM na Jumuiya zake kushiriki zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura linarotarajiwa kuzinduliwa tarehe 20 Julai mkoani Kigoma

Akizungumza leo Julai 10 baada ya kupokelewa na viongozi wa Serikali na Chama wilayani Igunga,Mwenyekiti Chatanda amesema kuwa Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni haki ya msingi kwa wananchi na kuwahimiza kushiriki utakapofika muda katika maeneo yao.

“UWT tumeanza ziara ya kuhamasisha wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa wale ambao hawajajiandikisha,”amesema.

kujitokeza kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Mwenyekiti Chatanda ameeleza kuwa msafara wake utajigawa katika maeneo tofauti ya mkoa wa Tabora na kufanya mikutano pamoja na kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here