Home KITAIFA MHANDISI MRAMBA AMEWATAKA TPDC KUONGEZA KASI YA USAMBAZAJI WA GESI

MHANDISI MRAMBA AMEWATAKA TPDC KUONGEZA KASI YA USAMBAZAJI WA GESI

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi TPDC kwa uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia.

Pia amewataka kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi hiyo kwa kushirikisha sekta binafsi.

Pongezi hizo ametoa Julai 9 2024 jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea banda la TPDC lilipo kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa amesema kufuatia na kuendelea na kukua kwa uchumi TPDC wanapaswa kuzishirikisha Sekta binafsi ili kuharakisha usambazaji wa gesi ya kupika majumbani unaenda kwa haraka.

“Kama tukiendelea kuwategemea TPDC peke yake katika usambazaji wa gesi ya kupikia tutachelewa sana kufikia malengo hivyo tunapaswa kuzishirikisha sekta binafsi ili kuharakisha mradi huu,”amesema Mhandisi Mramba.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa vituo vya kujazia gesi kwenye magari amesema serikali imejipanga kuongeza vituo nchi nzima ili kuhakikisha huduma inamfikia kila mwananchi.

“Tumejipanga kuhakikisha hivi vituo vya kujazia gesi vinaongezeka na kuwa vingi zaidi lakini pia tunampango wa kuanza kutumia magari maalumu yatakayotumika kama vituo vya kujazia gesi kwani malengo yetu mpaka kufikia mwaka 2025 kuwa na vituo zaidi ya 30 “,Amesema.

Ameongezq kuwa gari hizo maalumu zitakuwa zinapaki katika maeneo mbalimbali ambapo watu watakuwa wanafika na kujaziwa gesi kwenye vyombo vyao vya moto.

Mhandisi Mramba amewataka GASCO kutumia maonesho hayo kujitangaza kwani watu wengi hawajui wanachokifanya kwani wanachofanya kina umuhimu na tija kubwa kwa maslahi ya umma.

“Kuna wawekezaji wengi ambao wanakuja hapa nchini kujenga vituo vya mafuta lakini sijui kama wanawajua nyinyi mpo mnapaswa kujitangaza na kuelezea kazi zenu mnazozifanya ili watu hawa wanapokuja wakutane na nyinyi,”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here