Home AFYA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA TEMEKE YAIMARISHA HUDUMA KWA KUPOKEA MAGARI YA...

HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA TEMEKE YAIMARISHA HUDUMA KWA KUPOKEA MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA

Dar es Salaam

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa Temeke (TRRH) imepokea rasmi magari mawili ya kubeba wagonjwa, ambayo yamezinduliwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dorothy Kilave Ujio wa magari haya yanaenda kuboresha huduma za rufaa na za dharura zilizopo hospitalini hapo, na kufanya idadi ya magari ya kubeba wagonjwa kuwa matano.

Akizungumza Julai, 9 2024 jijini Dar es Salaam Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Joseph Kimaro, amethibitisha maboresho haya wakati akiwasilisha taarifa fupi ya utendaji kazi na maboresho katika hafla ya ugawaji wa magari ya kubeba wagonjwa mbele ya mgeni rasmi, Dorothy Kilave.

Dk. Kimaro ameeleza mafanikio mbalimbali ya hospitali hiyo moja ikiwa ni kununua kifaa tiba kinachoitwa laparoscopy tower, ambacho kitawezesha hospitali kufanya upasuaji kwa njia ya tundu ndogo, hivyo kupunguza rufaa ya wagonjwa kwenda katika hospitali za juu.

Aidha, kupitia utendaji mzuri wa timu ya uendeshaji wa huduma za afya, hospitali imeanza kutoa huduma za usafishaji damu (dialysis), na ndani ya wiki kadhaa imefanya sesheni 28 kwa wagonjwa nane waliopatiwa huduma.

Kwa upande wake, Dorothy Kilave amepongeza juhudi za hospitali katika kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi. Amesema kuwa kila anapofika hospitalini hapo anakuta kuna maboresho mapya ambayo wananchi wa Temeke wamekuwa wakiyatamani.

Ametoa shukrani na pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Rais kwa kusaidia na kusikiliza mahitaji ya majimbo mengi. Ameongeza kuwa, kwa siku ya leo, tunashuhudia Jimbo la Temeke likipokea vifaa hivi vya magari ya kubeba wagonjwa.

Pia, amehakikishia uongozi wa Hospitali juu ya uwepo wa fedha zitakazowezesha ujenzi wa gorofa sita litakalosaidia kupunguza na kuondoa changamoto ya ufinyu wa eneo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here