Home KITAIFA EWURA WANAFANYA VIZURI KUTOA LESENI NA VIBALI KWA WALE WANAOANZISHA ...

EWURA WANAFANYA VIZURI KUTOA LESENI NA VIBALI KWA WALE WANAOANZISHA VITUO VYA CNG.

Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wanafanya vizuri kutoa leseni na vibali kwa wale wanaoanzisha vituo Gesi Asilia Iliyogandamizi (CNG) ili jamii inufaike.

Hayo aliyasema Julai,9 2024 Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea banda la EWURA katika Maoneshoa ya 48 ya Biashara ya Kimataifa na amewapongezakwa majukumu wanayoetekeleza.

Amesema wanahakikisha udhibiti wa bei ya bidhaa, huduma yenyewe inapatikana na kudhibiti ubora wa huduma na kuhusu udhibiti wa bei ya bidhaa, Tanzania ni nchi ambaye bei za nishati ya umeme zipo chini zaidi.

“Nchi yetu ni yenye bei ya chini ya umeme, hata ukilinganisha na nchi majirani zetu utabaini hili.Upatikanaji wa huduma hii umeimarika sana, hatusemi kwamba ubora umetulia mahali ambapo hamna shida, hapana ila angalia tupo kwenye ubora mzuri,” amesema Mhandisi Mramba.

Amesema serikali inaendelea kuisimamia vyema mamlaka hiyo ili itekeleze vyema majukumu yake na zipo huduma za kiushauri na malalamiko ambazo EWURA wanatoa kwa wananchi ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa EWURA, Dk. James Andilile, amesema wataendelea kuhakikisha huduma wanazotoa za umeme na gesi asilia zinaendelea kupatikana katika ubora unaotakiwa.

Amesema wanaeendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya uwekezaji na mwezi uliopita walitiana saini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupimana utendaji kazi na wanatekeleza majukumu mbalimbali ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya umeme hususani Mradi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa upande wa sekta ya mafuta, amesema wanaendelea kufuatilia ubora wa mafuta na hadi Juni 30 habari ya ubora wa mafuta ulikuwa umefikia asilimia 97.

Amesema lengo ni kuhakikisha mafuta yanauzwa kwenye ubora unaotakiwa na kufuatilia mwenendo wa bei za soko la dunia ili kuangalia unafuu wa bei kwa wananchi.

Ameahidi kuendelea kutoa bei za kila mwezi na kwamba wamegeukia pia gesi ya kwenye magari na kuwapo kwake kumasaidia kupunguza matumizi ya Dola nchini kwasababu huduma hiyo inapatikana Tanzania.

Kuhusu sekta ya maji amesema wanaendelea kufuatilia upatikanaji wa huduma na kila eneo serikali inafanya uwekezaji ambao utasaidia kuwa na huduma za kutosha na Jukumu lao ni kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za maji kila sehemu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here